Picha ya kiazi yauzwa kwa dola milioni moja

Image caption Picha ya kiazi yauzwa kwa dola milioni moja

Sio jambo la ajabu kutamani kula viazi hususan baada ya kubugia glasi kadha ya mvinyo.

Iwe ni viazi karai ,viazi vya kuchoma au hata Chips lakini bwana mmoja nchini Uingereza ameustaajabisha ulimwengu kwa kununua picha ya kiazi kwa dola milioni moja.

Baada ya kumimina glasi kadhaa za kinywaji chake alitia sahihi hundi ya pauni laki saba u nusu £750,000 sawa na dola dola milioni moja za Marekani $1066199.97.

Mpiga picha Kevin Abosch aliiambia jarida la The Sunday Times

''sio mara ya kwanza kwa mtu aliyebugia kiileo chake kununua picha aliyoangika ukutani''

''tulikuwa tumekunywa glasi mbili za mvinyo,,nilifurahi sana.'

''Lakini baada ya glasi zingine mbili za mvinyo bwana huyo alinisisitizia kuwa ,kwa kweli naipenda sana picha hiyo sijui iwapo unaweza kuniuzia hiyo''

Haki miliki ya picha PABLO MARTINEZ MONSIVAIS AFP Getty Images
Image caption Bei ya picha zake huwa ni takriban dola 285,00 au pauni £200,000.

''Baada ya majuma mawili tulikubaliana bei yake na malipo yakafanywa''

Abosch aliipiga picha kiazi hicho kutoka ulaya mwaka wa 2010 kama mojawepo ya msururu wa viazi asilia.

Alipata umaarufu mkubwa kwa kuwapiga picha wasanii maarufu Johnny Depp na muigizaji na mtayarishaji nyota Steven Spielberg.

Bei ya picha zake huwa ni takriban dola 285,00 au pauni £200,000.

Picha hiyo iliambatana na viazi asilia na mboga .