Matokeo ya uchaguzi wa ubunge yafutwa CAR

uchaguzi Haki miliki ya picha AFP
Image caption Duru ya pili ya uchaguzi itafanyika 7 Februari

Mahakama ya kikatiba nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imefuta matokeo yote ya uchaguzi wa ubunge kutokana na kasoro nyingi zilizotokea wakati wa uchaguzi.

Mahakama hiyo hata hivyo imeidhinisha matokeo ya uchaguzi wa urais, ambao ulifanyika karibu mwezi mmoja uliopita.

Imethibitisha kwamba mawaziri wakuu wa zamani Anicet-Georges Dologuele na Faustin Touadere watakutana kwenye duru ya pili ya uchaguzi tarehe 7 Februari.

Tarehe ya kurudiwa kwa uchaguzi wa ubunge haijatangazwa.

Wagombea urais wapinga uchaguzi CAR

Kwenye uchaguzi wa duru ya kwanza, Anicet-Georges Dologuele alipata 23.74% ya kura naye Faustin Touadera akapata 19.50 %.

Kulikuwa na wagombea 30 waliopigiwa kura na takriban wapiga kura 2 milioni kwenye uchaguzi huo uliotarajiwa kurejesha uthabiti katika taifa hilo.

Haki miliki ya picha AFP

Walinda amani 11,000 wa Umoja wa Mataifa wakisaidiana na mamia ya wanajeshi wa mkoloni wa zamani Ufaransa wamekuwa wakijaribu kudumisha amani nchini humo.