Rihanna na Kanye West watoa albamu mpya

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Rihanna

Ni miaka minne tangu nyota wa muziki Rihhana atangaze kwamba anaanda albamu yake mpya.

Hatahivyo harakati hizo zilikabiliwa na changomoto chungu nzima na kulazimika kuchelewesha utayarishaji wake.

Lakini hatimaye ndoto yake imefaulu na sasa albamu hiyo ya nane kwa jina ANTI imekamilika.

Nyota huyo alifanya tangazo hilo akiwa amevaa taji la dhahabu la malkia pamoja na vipaza sauti vya masikioni vya Dolce na Gabbana.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kanye West

Wakati huohuo albamu mpya ya nyota Kanye West 'SWISH' ilitarajiwa kuwa tayari kwa onyesho lake la Glastonbury wakati wa msimu wa joto uliopita.

Hatahivyo mpango huo haukufaulu huku nyota huyo wa muziki wa rap akiambia Vanity Fair kwamba alikuwa anaichelewesha kwa makusudi.

Lakini usiku wa jana alitangaza kwamba albamu hiyo iko tayari.