Mhamiaji aliyeua akamatwa Sweden

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mhamiaji mwenye umri wa miaka 15 amekamatwa kwa mauaji ya mfanyikazi wa kike katika kambi ya wakimbizi.

Polisi nchini Sweden wamemkamata mhamiaji mwenye umri wa miaka 15 kwa mauaji ya mfanyikazi wa kike katika kambi ya wakimbizi.

Mfanyikazi huyo, 22 alidungwa kisu na kuuawa katika kambi hiyo inayowahifadhi wakimbizi watoto wasioandamana na wazazi mjini Molndal karibu na eneo la Gothenburg.

Waziri mkuu wa Sweden alizuru kambi hiyo na kulaani mauaji hayo akisema raia wengi wa Sweden wanahofia kushambuliwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kijana mhamiaji aliyeua akamatwa Sweden

Sweden iliwakaribisha wakimbizi wengi mwaka uliopita na mamlaka ya uhamiaji imesema visa vya mashambulizi katika vituo vya kuwasajili wahamiaji vimeongezeka maradufu.