Polisi sita wafutwa kazi Ohio

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maafisa wa polisi wakifanya msako katika mji wa Ohio nchini Marekani

Maafisa wa polisi katika mji wa Cleveland, Ohio, wamewafuta kazi maafisa sita waliowafyatulia risasi zaidi ya watu 100 katika gari na kuwauwa wachumba wawili weusi mwaka 2012.

Maafisa waliofutwa kazi ni Michael Brelo, aliyeondolewa mashtaka ya kuuwa bila kukusudia mwaka uliopita.

Maafisa wengine sita watasimamishwa kazi kwa siku 21 hadi 30.

Ufyatuaji huo unafuatia msako uliohusisha magari ya polisi 62 na Zaidi ya polisi 100.

Steve Loomis, rais wa chama kikubwa cha polisi mjini humo amesema atapinga kufutwa kazi kwa maafisa hao.

Kisa hicho kilianza wakati gari bovu lilianza kutoa mlio kama wa risasi. Ilisababisha kifo cha Timothy Russell, aliyepigwa risasi 24 na Malissa Williams,aliyepigwa 23.

Maafisa kadhaa walifyatua lakini ni Brelo ndiye aliyeshtakiwa.