Sudan yafungua mpaka wake na Sudan Kusini

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Omar al Bashir

Rais wa Sudan Umar al-Bashir ametoa agizo la kufunguliwa kwa mpaka kati ya taifa hilo na lile la Sudan Kusini.

Bashir pia ametoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua zote ili kuhakikisha kuwa agizo hilo linaidhinishwa.

Sudan ilifunga mpaka wake na Sudan Kusini mnamo mwezi Juni 2011,mwezi mmoja kabla ya kutangazwa rasmi kwa Uhuru.

Wakati huo,uamuzi huo ulianza kutekelezwa baada ya kuanza kwa uasi kusini mwa Kordofan uliotekelezwa na vuguvugu la SPLM kaskazini.

Baadaye Khartoum iliishtumu Juba kwa kuunga mkono wanachama wa zamani wa chama tawala nchini Sudan Kusini.

Wiki iliopita,Bashir aliagiza kupunguzwa kwa kodi ya kusafirisha mafuta yanayotoka Sudan Kusini.

Siku ya jumatatu,Rais Salva Kiir alijibu kwa kuliagiza jeshi lake kuondoka katika mpaka na Sudan na kukaa umbali wa kilomita nane.