Syria:Waasi na wapinzani wakutana Saudia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mapipigano nchini Syria

Muungano wa wawakilishi wa waasi nchini Syria na makundi ya upinzani yanakutana katika mji mkuu wa Saudi Arabia Riyad, kujadili ikiwa watahudhuria mazungumzo ya amani mjini Geneva baada ya wiki hii au la.

Muungano huo unaoungwa mkono na Saudia, umekuwa ukishinikiza kusitishwa kwa mashambulio ya mabomu na kutwaliwa kwa maeneo ya raia kabla mazungumzo yoyote na rais Bashar al Assad kuanza.

Juhudi hizo za umoja wa mataifa zimejiri huku wanajeshi wa serikali ya Syria, kwa ushirikiano na wanajeshi wa Urusi, wakiendelea kutwaa maeneo zaidi yaliyokuwa yakithibitiwa na waasi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Makundi mbalimbali ya Syria yakutana Saudia

Chama kikuu cha Kikurdi nchini Syria PYD, kimesema kuwa hakijaalikwa kwenye mazungumzo hayo baada ya serikali ya Uturuki kupinga kujumuishwa kwao.