Kituo cha habari chalalama kuhusu Trump

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Donald Trump asusia mdahalo wa Fox News

Kituo cha habari nchini Marekani Fox News kimemlalamikia mgombea wa Urais wa chama cha Republican Donald Trump baada ya hatua yake kukataa kushiriki mdahalo wa wagombea wa chama hicho utakaofanyika kwenye runinga hiyo.

Fox News imemlaumu Bw Trump kwa kumshambulia msimamizi wa mjadala Megyn Kelly na kwamba meneja wa kampeni ya Trump amekuwa akimtishia Bi Kelly.

Dunald Trump ametaka Bi Kelly kuondolewa kama msimizi akisema amekua akimuonea baada ya wawili hao kujibizana vikali kwenye mdahalo wa mwezi Agosti mwaka uliopita.