Wahamiaji 24 wafa maji karibu na Ugiriki

Image caption Wahamiaji 24 wafa maji karibu na Ugiriki

Wahamiaji 24 wamekufa maji baada ya boti walimokuwa, kuzama karibu na kisiwa cha Samos kilichoko Ugiriki mkabala na Uturuki.

Watu wengine 11 waliokolewa.

Waokoaji wanaendelea kutafuta miili ya watu wengine 11.

Watoto kadhaa walikuwa miongoni mwa wahasiriwa kulingana na walinzi wa ufukweni wa Ugiriki.

Hii ni ajali ya pili katika siku mbili.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu wengine 11 waliokolewa.

Wahamiaji wengine 7 walikufa maji karibu na kisiwa cha Kos kilichoko Ugiriki siku ya Jumatano.

Hadi kufikia leo takwimu zinaonesha kuwa takriban watu 200 wamepoteza maisha yao wakijaribu kuingia bara Ulaya mwezi huu pekee.

Hadi kufikia tulipochapisha habari hii, uraia wa wahasiriwa haukuwa umebainika.

Umoja wa Ulaya umetoa ilani kwa Ugiriki likiitaka iimarishe ulinzi wa mika yake la sivyo hatua za pamoja zitumiwe dhidi yake.

Maafisa wa uhamiaji wa Ulaya wametumwa katika eneo la Samos kujaribu kudhibiti hali na kuwaokoa watu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Inakisiwa kuwa takriba wakimbizi 850,000 waliwasili Ugiriki mwaka uliopita.

katika mpango huo, wahamiaji watakaowasili katika visiwa vya Ugiriki, watafurushwa kwa feri kurudishwa uturuki ambayo ndio inayotumika kama kiingilio kikuu cha wahamiaji na wakimbizi.

Mpango huu mpya unawapa kipao mbele wahamiaji na wakimbizi walioko Uturuki.

Wahamiaji 250,000 kati yao watakuwa wakiruhusiwa kuingia bara Ulaya kila mwaka.

Inakisiwa kuwa takriba wakimbizi 850,000 waliwasili Ugiriki mwaka uliopita.