Joseph Fiennes amuigiza Michael Jackson

Haki miliki ya picha APReuters
Image caption Joseph Fiennes

Muigizaji wa filamu kutoka nchini Uingereza Joseph Fiennes, amekiri kuwa alishangazwa na kitendo cha kumuigiza mfalme wa muziki aina ya POP, Michael Jackson katika mchezo wa runinga ,baada ya kukosekana kwa muigizaji mweupe.

Muigizaji huyu atakayeigiza kama mwanamuziki katika vichekesho vinavyorushwa na mtandao wa ''sky network" unaohusu safari ya barabarani iliyofanywa na Michael Jackson na marafiki zake kina Marlon,Brando na Elizabeth Taylor baada ya uvamizi wa mara 9-11.

Fiennes alieleza kuwa tabaka hilo la kati halikuwa chaguo lake lakini alisema Michael Jackson alikuwa na tatizo la rangi yake ngozi kutokuwa ya asili,hivyo suala la utofauti wa rangi halikuwa kikwazo kwake .