Netflix yazimiwa huduma Indonesia

Haki miliki ya picha
Image caption Netflix yazimwa Indonesia

Siku chache tu baada ya Halmashauri ya kudhibiti video na filamu nchini Kenya (KFCB) kupinga hatua ya kampuni ya Netflix kuanza kutoa huduma zake nchini Kenya, kampuni hiyo ya Marekani imepata pigo kubwa nchini Indonesia baada ya kampuni moja inayotoa huduma ya mtandao wa Intaneti kuiondoa kwenye huduma zake.

Kampuni hiyo ya kutoa huduma ya mtandao wa intaneti ilieleza kuwa iliizima Netflix kwa sababu iligundua kampuni hiyo inayotoa huduma ya video na filamu kupitia mtandao wa intaneti haikuwa ni vibali mahsusi za kupeperusha matangazo yake nchini Indonesia.

Kampuni hiyo inamilikiwa na serikali.

Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Reed Hastings alitangaza upanuzi huo katika maonyesho ya teknolojia ya CES mjini Las Vegas nchini Marekani majuma mawili yaliyopita.

Mataifa pekee ambayo Netflix haijafanikiwa kuingia ni Uchina, Korea Kaskazini, Syria na Crimea.

Maafisa wa Telekom Indonesia wamesema kuwa Netflix inapaswa kujadiliana nao kuhusu mbinu za kutathmini ubora na viwango vya filamu na video zinazopeperushwa kwenye mitandao yake.

''Tatizo letu kubwa idhini. Netflix haijapata idhini ya kutupa matangazo yake hapa Indonesia. Alisema waziri wa mawasiliano wa Indonesia Rudiantara.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Netflix haijaeleza inapanga kushughulikia vipi matakwa haya ya serikali mbalimbali.

''Haitakubalika kwao (Netflix) kutupa picha chafu bila vidhibitio ni kinyume cha sheria.'' alisema mkurugenzi wa matumizi Dian Rachmawan

Indonesia ni moja katia ya mataifa ya bara Asia yenye idadi kubwa zaidi ya watu ikiwa na watu 250.

Mbinu itakayotatua mzozo huo unatarajiwa kutazamwa kwa kurunzi nchini China ambapo Netflix imewasilisha ombi la kutaka ianze kupeperiusha matangazo yake huko.

Serikali ya Vietnam vilevile imetoa ilani kwa Netflix itafute idhini rasmi kabla haijaanza kupeperusha matangazo yake nchini humo.