Sweden kuwafurusha wahamiaji 80,000

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahamiaji Sweden

Mamlaka nchini Sweden imeanza mpango wa kuwafurusha takriban wahamiaji 80,000,waziri wa maswala ya ndani amenukuliwa akisema.

Anders Ygeman amesema ndege itatumiwa kuwarudisha wahamiaji hao lakini itachukua miaka kadhaa.

Takriban wahamiaji 163,000 walituma maombi ya uhamiaji nchini Sweden mwaka 2015,ikiwa ni idadi ya juu barani Ulaya.

Idadi hiyo imeshuka sana tangu Sweden iweka sheria kali za kudhibiti mipaka yake mwaka huu.

Pamoja na Ujerumani mataifa yote ya Scandinavia ni maeneo yanayopendwa sana na wahamiaji wanaoingia barani Ulaya kinyume na sheria.

Kati ya visa 58,800 vya wahamiaji vilivyoangaziwa mwaka uliopita,asilimia 55 ya visa hivyo vilikubaliwa.

Kati ya wale ambao huenda wakafunrushwa,Bw.Ygeman amenukuliwa katika vyombo vya habari nchini Sweden akisema kuwa wahamiaji hao ni 60,000 lakini idadi hiyo inaweza kupanda hadi 80,000.