Bondia Fury aonywa dhidi ya matamshi ya kukera

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bondia Fury aonywa dhidi ya matamshi ya kukera

Bondia Muingereza Tyson Fury ameonywa na mahakama nchini Uingereza kuwa atachukuliwa hatua za kinahamu endapo ataendelea kutoa matamshi yenye utata yasiohusiana na ndondi.

Bingwa huyo wa uzani mzito alionywa katika mkutano wa nidhamu na halmashauri inayosimamia ndondi nchini Uingereza.

Fury, 27, alilazimika kuomba msamaha kwa yeyote aliyemkwaza baada ya kuwatusi wanawake na wapenzi wa jinsia moja.

Takriban watu 140,000 walitia sahihi shinikizo la kutaka aondolewe kwenye kinyang'anyiro cha kuwani tuzo la mwanaspoti bora nchini Uingereza mwezi Desemba mwaka uliopita.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bondia Tyson Fury aligonga vichwa vya habari baada ya kumtamausha mshikilizi wa mataji yote makuu ya ndondi Wladimir Klitschko kutoka Ukraine mwezi Novemba kwa wingi wa pointi.

Bondia huyo mwenye asili ya Manchester aligonga vichwa vya habari kote duniani baada ya kumtamausha mshikilizi wa mataji yote makuu ya ndondi Wladimir Klitschko kutoka Ukraine mwezi Novemba kwa wingi wa pointi.

Kulingana na shirikisho hilo linalosimamia maswala ya nondi nchini Uingereza BBBC, bondia huyo hakuvunja sheria yeyote ila

'' Baada ya kumchapa Wladimir Klitschkoto, Fury alitoa matamshi yaliyochukiza sana wapenzai wa jinsia moja na wanawake ila kwa kufanya hivyo alikuwa akijieleza kama inavyoruhusiwa katika katiba ya taifa kwa hivyo hatutamchukulia hatua ila tumempa onyo'' ilisema taarifa hiyo kutokla kwa shirikisho la ndoni la Uingereza.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Pigano la marudiano limepangwa kufanyika baadaye mwaka huu.

''Fury sasa amefahamishwa kuwa bondia bingwa ina majukumu makubwa ambayo yanapaswa kumzuia kuwaudhi watu mbali na kuwajibikia jamii pasi na kutoa matamshi yasioendana na ndondi'' taarifa hiyo iliyoongezea.

Pigano la marudiano limepangwa kufanyika baadaye mwaka huu.