Makundi yatishia kutohudhuria mkutano Syria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wapiganaji wa Syria

Mazungumzo ya amani kuhusu Syria yanatarajiwa kuanza mjini Geneva huku kukiwa na mkanganyiko kuhusu iwapo makundi ya upinzani yatahudhuria.

Awali ,baadhi ya viongozi wa upinzani walisema kuwa wawakilishi wengine hawatahudhuria hadi pale hatua zitakapochukuliwa kusitisha ulipuaji wa raia,lakini afisa mwengine mwandamizi amesema kuwa watahudhuria.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption vita vya Syria

Ujumbe wa serikali ya Syria unatarajiwa kuwasili Geneva baadaye.

Katika ujumbe wa video uliotumwa kwa raia wa Syria,mjumbe wa umoja wa mataifa Steffan de Mistura amesema kuwa mazungumzo hayo hayawezi kufeli.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mkutano Syria

Zaidi ya watu 250,000 wamefariki katika miaka mitano ya vita nchini Syria.

Watu wengine milioni 11 wamelazimika kutoroka makwao huku wanajeshi waliowatiifu kwa rais Bashar Al Asaad na wengine wanaopinga utawala wake wakikabiliana,pamoja na wapiganaji wa jihadi kutoka kundi la Islamic State.