Njaa yawaua watu 16 Syria

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wakimbizi wa Syria

Shirika la Matabibu la Kimataifa, MSF, linasema kuwa watu 16 wengine wamekufa kwa njaa, katika mji uliozingirwa wa Madaya, nchini Syria, tangu msafara wa msaada kuruhusiwa kuingia katika mji huo mwezi huu.

MSF imesema kuna watu zaidi ya mia tatu wanaotapia mlo mjini humo, na watu kama 30 huenda wakafa.

Ripoti ya MSF imetoka wakati mazungumzo ya kujaribu kumaliza vita vya miaka mitano vya Syria, yanafanywa mjini Geneva, Uswizwi.

Wapatanishi wanaowakilisha makundi makuu ya upinzani ya Syria, wanatarajiwa Geneva hii leo, baada ya kususia mwanzo wa mazungumzo hayo hapo jana.