Ufaransa kuondoa majeshi yake Jamhuri ya Kati

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ufaransa kuondoa majeshi yake Jamhuri ya Kati

Ufaransa itaondoa majeshi yake katika Jamhuri ya Afrika ya Kati mwaka huu.

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, amesema Ufaransa inalenga kumaliza operesheni zake za kijeshi katika taifa hilo lilolozongwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Waziri Le Drian alisema hali ya usalama imeimarika.

Hata hivyo vikosi vidogo vya majeshi ya Ufaransa vitabakia nchini humo, kama ilivyokuwa kabla ya ghasia za wenyewe kwa wenyewe kutibuka nchini humo miaka mitatu iliyopita.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waziri Le Drian alisema hali ya usalama imeimarika.

Mwaka jana, Ufaransa ilianzisha uchunguzi kuhusu unyanyasaji wa kijinsia uliofanywa na askari wake wa kulinda amani .

Madai kama hayo pia yameibuka dhidi ya walinda amani wa umoja wa mataifa na majeshi mengine ya muungano wa ulaya.

Walinda usalama hao walikuwa wameenda huko kuwagawanya waasi waislmu na makundi ya wapiganaji wakristu almaarufu Anti-Balaka.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hata hivyo vikosi vidogo vya majeshi ya Ufaransa vitabakia nchini humo

Vita nchini humo vilianza baada ya Muungano wa viongozi wa kanda ya Afrika ya Kati kumuagiza rais Mitchel Djotodia na wapiganaji wa Seleka kunga'tuka madarakani na kusababisha wakristu waliokuwa na hasira kuwashambulia waisilamu wakilipiza kisasi ya mauaji mikononi mwa waasi wa Seleka.

Maelfu ya watu walipoteza maish yao huku mapigano yakichukua mkondo wa kikabila.