Takriban Watu 50 wauawa Syria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kundi la wanamgambo IS linadaiwa kuhusika na shambulio hilo

Takriban watu 50 wameuawa kwa mlipuko wa bomu karibu na hekalu la kishia la Sayyida Zeinab,kusini mwa mji wa Damascus nchini Syria.

Kituo cha basi na Jengo lililo na makao makuu ya jeshi vilishambuliwa na milipuko ambayo iliharibu magari yaliyokuwepo katika eneo hilo.

Ilitokea wakati Serikali na makundi ya upinzani walipokutana mjini Geneva kwa ajili ya mazungumzo yenye kulenga kupata suluhu ya kisiasa kuhusu mzozo wa nchini humo.

Shambulio hilo linadaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State, ambalo linaelezwa kulenga kuvuruga mazungumzo hayo, Umoja wa Ulaya umeeleza.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry amezisihi pande zote mbili kukomesha vitendo vya umwagaji damu.

Mjumbe wa Umoja wa mataifa nchini Syria amepanga kufanya mazunguzo na pande mbili mjini Geneva, Jumatatu