50 wauawa katika milipuko Syria

Haki miliki ya picha EPA
Image caption 50 wauawa katika mashambulizi Syria

Milipuko kadha ya mabomu imeuwa watu kama 50, na kujeruhi zaidi ya watu mia moja, katika mtaa wa Sayida Zeinab, kwenye vitongoje vya Damascus.

Eneo lililoathirika na mshambulizi hayo lipo karibu na pahala takatifu kabisa nchini Syria, kwenye madhehebu ya Shia.

Kundi la Islamic State linasema limefanya shambulio hilo

Eneo lililoshambuliwa la Sayidna Zeinab linaaminika kuwa na kaburi la bintiye mtume Mohammed.

Vilevile linaaminika kuwa na mabaki ya mwanawe Ali ambaye wafuasi wa dhehebu la Shia wanaamiini ndiye mrithi wa mtume Mohammed.

Haki miliki ya picha
Image caption Bashar al Jaafari, kiongozi wa ujumbe wa serikali ya Syria anasema shambulio hilo linathibitisha uhusiano baina ya upinzani na ugaidi.

Mwandishi wa habari wa BBC aliyefika pahala hapo , anasema kuna majengo yanayowaka moto na magari yaliyoteketea.

Bashar al Jaafari, kiongozi wa ujumbe wa serikali ya Syria katika mzungumzo ya amani ya Syria mjini Geneva, anasema shambulio hilo linathibitisha uhusiano baina ya upinzani na ugaidi.