Karibu simba 100 wagunduliwa Ethiopia

Image caption Idadi ya Simba barani Afrika imepungua kwa nusu tangu miaka ya tisini.

Idadi fulani ya simba ambayo haijulikani ya takriban simba 100 wamegunduliwa na shirika moja na wanyamapori katika mbuga moja iliyo mbali kaskazini magharibi mwa Ethiopia.

Wakfu wa Born Free unasema kuwa umepata picha na kutambua njia za simba katika eneo la Alatash liilo karibu na mpaka na Sudan.

Eneo hilo linaaminika kupoteza simba wake wote katika karne ya 20 kutokana na kuwindwa na kuharibiwa wa mazingira yao.

Idadi ya Simba barani Afrika imepungua kwa nusu tangu miaka ya tisini.

Simba hao wanaaminiwa kutoka kwa familia moja ya simba kutoka nchini Jamhuri ya Afrika ya kati ambapo ni simba 900 waliaminika kunusurika.

Uwepo wa Simba katika eneo la Alatash haiujathibitishwa rasmi kwenye mikutano ya kitaiafa na kimataifa kwa mijibu wa mtaalamu wa masuala ya simba kutoka chuo cha Oxford.