Wanasayansi waruhusiwa kubadili DNA

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Utafiti huo utafanyika siku saba za kwanza baada ya kukutana kwa chembe chembe za mme na mke

Wanasayansi nchini Uingereza wamepewa idhini na idara inayohusika na masuala ya uzazi ya kufanyia viinitete vya binadamu mabadiliko ya kijenetiki.

Wanasayansi hao watafanya utafiti huo katika taasisi ya Francis mjini London.

Utafiti huo una lengo la kutoa uelewa kamili kuhusu siku za kwanza kwanza katika maisha ya binadamu.

Utaanza siku saba za kwanza baada ya kukutana kwa chembe chembe za mme na mke na kuonyesha kile ambacho husababisha mimba kutoka.

Mwaka uliopita wanasayansi nchini China walitangaza kuwa walifanyia mabadiliko ya kijenetiki viini tete vya binadamu kurekebisha hali ambayo husababisha tatizo la damu.

Hatua hiyo imezua maoni tofauti huku baadhi wakisema kuwa kuifayika mabadiliko DNA ni hatua ambayo imeenda mbali zaidi na huenda ikasababisha kuzaliwa watoto waliotengezezwa.