AS Roma yamsajili Doumbia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Doumbia alifunga magoli 66 katika mechi 108 akiwa na klabu ya CSKA

Klabu ya Newcastle imemsajili mshambuliaji raia wa Ivory Coast Seydou Doumbia kwa mkopo kutoka klabu ya AS Roma.

Mcheza soka huyo wa umri wa miaka 28 alihamia klabu ya Roma Januari mwaka 2015 kwa kima cha pauni millioni kumi.

Lakini alicheza tu mara 13 kabla ya kuhamia klabu ya CSKA ya Moscow kwa mkopo kwa mara ya pili.

Doumbia alifunga magoli 66 katika mechi 108 kwa klabu hiyo ya Urusi.

Amekuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Newcastle mwezi Januari na kujiunga na wachezaji wa kiungo cha kati wakiwemo Jonjo Shelvey, Andros Townsend na Henri Saivet.