Vizuizi kwenda Ramallah vyaondolewa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Israeli imejikakamua kusitisha visa vya uchomaji visu, kupigwa risasi na kugongwa na magari.

Jeshi la Israeli limeondoa vizuizi kwenda mji wa ukingo wa magharibi wa Ramallah vilivyowekwa baada ya ufyatuaji wa risasi wa siku ya Jumapili.

Wasio wenyeji walizuiwa siku ya Jumatatu kuingia katika mji huo ambapo uliko utawala wa Palestina.

Wakati wa shambulizi hilo la Jumapili polisi mpalestina aliwapiga risasi na kuwajeruhi wanajeshi wawili wa Israeli nje ya mji wa Ramallah.

Israeli imejikakamua kusitisha visa vya uchomaji visu, kupigwa risasi na kugongwa na magari, vinavyoendeshwa na wapalestina na waisraeli ambavyo vimesababisha vifo vya waisreali 28 tangu mwezi Oktoba

Zaidi ya wapalestina 158 wengi wao washambuliaji nao wameuawa katika kipindi hicho.