Jordan yalemewa na wakimbizi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mfalme Abdullah wa Jordan

Mfalme Abdullah wa Jordan anasema kuwa nchi yake iko kwenye hatari kubwa kufuatia wimbi la maelfu ya wakimbizi kutoka nchini Syria.

Kabla ya kufanyika kwa mkutano kuhusu utoaji misaada nchini Syria, mfalme Abdullah aliiambia BBC kuwa kuna shinikizo kubwa katika utoaji wa huduma za kijamii nchii Jordan, za miundo msingi na kwa uchumi.

Amesema kuwa jamii ya kimataifa inahitaji kutoa usaidizi zaidi ikiwa itahitaji Jordan iendelee kuwachukua wakimbizi zaidi.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Jordan imewahifadhi wakimbizi 635,000 kutoka nchini Syria

Umoja wa Mataifa unatafuta dola billioni 7.7 kufadhili oparesheni za kutoa misaada kwa watu milioni 22.5 nchini Syria na nchi majirani mwaka ujao.

Jordan inawahifadfhi watu 635,000 kati ya watu millioni 4.6 ambao ni wakimbzi raia wa Syria waliosajiliwa na Umoja wa Mataifa. Serikali inasema kuwa zaid ya watu milioni moja raia wa Syria wanaoishi nchini humo wakiwemo wale waliowasilii kabla ya mzozo kuanza mwaka 2011.