Brazil kutokomeza virusi vya Zika

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Brazil imeapa kupambana dhidi ya virusi vya Zika

Rais wa Brazil Dilma Rousseff amesema Serikali inalenga kutokomeza Mbu wanaosambaza virusi vya Zika.

Akizungumza kwenye Bunge la Congress katika mwanzo wa mwaka wa kikao hicho nchini humo,Rais Rousseff amesema pesa zitatengwa kwa ajili ya mpango huo.

Pia amesema Brazil na Marekani zinashirikiana ili kuweza kupata chanjo dhidi ya virusi ambavyo vimehusishwa na kesi nyingi za kuzaliwa kwa watoto walio na dosari kwenye ubongo.

Miezi sita ijayo michuano ya Olimpiki itafanyika jijini Rio.

Mkurugenzi wa Kamati ya maandalizi, Mario Andrada ameiambia BBC kuwa ana uhakika kuwa virusi hivyo havitakuwa tishio kwa wale watakaoingia Brazil kushuhudia michezo hiyo.