Watu wafa njaa Sudan Kusini

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Makamu wa rais wa zamani Riek Machar na rais Salva Kiir

Watu wanaripotiwa kutaabika kutokana na njaa katika eneo la Western Equatoria nchini Sudan Kusini, wakati ambapo pande mbili hasimu katika vita vya wenyewe kwa wenyewe zikichelewa kutekeleza mpango wa amani.

Akinukuliwa na vyombo vya habari rais wa zamani wa Botswana Festus Mogae ambaye ni kiongozi wa kundi linalofuatilia mpango huo amewaambia wakiishi wa seriali na wa waasi kuwa hali inazidi kuwa mbaya

Kundi moja la waanngalizi linasema kuwa lilipata watu wenye njaa katika eneo la Mudri lililo Western Equatoria.