Wasifu wa seneta Ted Cruz

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ted Cruz alizaliwa mwaka 1970

Wengi wamekuwa wakisema kuwa Seneta Ted Cruz ndiye pekee anaweza kumshinda Donald Trump kwenye uteuzi wa chama cha Republican.

Cruz ambaye ni seneta kutoka jimbo la Texas, tayari alionyesha dalili mapema baada ya kuibuka mshindi katika uteuzi wa jimbo la Iowa. Lakini katika hatua ya kushangaza, alijitoa kwenye kinyang'anyiro baada ya kushindwa kwenye mchujo jimbo la Indiana.

Wakati wa kipindi chake kifupi katika siasa, Cruz mwenye umri wa miaka 46 anatajwa kama mtu aliyechukuwa sana huku Washington kutokana na siasa zake na ambaye mara nyingi hukorofishana na chama chake binafasi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Donald Trump na Ted Cruz

Rafael Edward Cruz alizaliwa mwaka 1970 eneo la Calgary nchini Canada suala ambalo huenda likaja kutumiwa kumpinga.

Mamake alikuwa raia wa Marekani jambo lililompa uraia mara mbili wa Marekani na Canada huku babake akiwa ni mhamiaji kutoka nchini Cuba ambaye aliingia nchini Marekani kukimbia utawala wa Batista.

Familia ya Cruz ilihamia Houston huko Texas mwaka 1974 ambapo akiwa na umri wa miaka mitatu alipewa jina Ted.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Aligombea na kushinda kiti cha Seneta katika jimbo la Texas mwaka 2012

Alihudhuria masomo yake katika chuo cha Prince University ambapo alikuwa maarufu wa midahalo na kisha kuelekea chuo cha Harvad kusomea masuala ya sheria.

Bwana Cruz alihudumu kama karani wa mkuu wa sheria katika mahakama kuu mwaka 1996 na kisha kujiunga na kampuni moja ya masuala ya sheria mjini Washington DC ambapo alishughulikia kesi kubwa.

Alikutana na mkewe Heidi Nelson wakati wote hao walikuwa washauri kwenye kampeni ya George W Bush mwaka 2000 na wamebarikiwa na watoto wawili wasichana.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Amesomea taaluma ya sheria

Mwaka 2012 aligombea kiti cha Useneta katika jimbo la Texas dhidi ya mgombea maarufu. Hata hivyo aliibuka mshindi na ndio wakati wa kwanza bwana Cruz alishikilia ofisi ya umma.

Bwana Cruz alitangaza azimio lake la kugombea urais wa mwaka huu wa 2016 katika chuo cha Christian Liberty. Aliahidi kuwadirusha watu makwao na kuboresha usalama katika mpaka wa Marekani na Mexico.