Mkuu wa mashtaka akamatwa Zimbabwe

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe

Mwendesha mashtaka mkuu nchini Zimbabwe Johannes Tomana amekamatwa na polisi na atarajiwa kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa gazeti la serikali la Herald

Gazeti hilo linasema kuwa mashtaka yanayomkabili bado hayajulikani lakini inaaminika kwa hilo ni kuhusiana na na kufutwa kwa mashtaka wiki iliyopita yaliyokuw yakiwakabili watu wawili ambao wanashutumiwa kwa kupanga njama ya kulipua kiwanda cha maziwa cha rais Robert Mugabe.