Wataka viongozi wa mapinduzi wafungwe maisha Burundi

Image caption Aliyekuwa waziri wa ulinzi Cyrille Ndayirukiye

Mawakili wa upande wa mashtaka nchini Burundi wamekata rufaa dhidi ya uamuzi uliopewa viongozi wa jaribio la mapinduzi,wakitaka wote wapewe hukumu ya maisha jela,kulingana na chombo cha habari cha AFP.

Pia walipata orodha ya viongozi 34 wa upinzani waliokwenda mafichoni,wanaharakati na waandishi ambao wanataka kuwashtaki kwa jukumu lao katika jaribio la mapinduzi hayo ya mwezi May 2015.

Rufaa hiyo inajiri baada ya mahakama mwezi uliopita kuwahukumu kifungo cha miaka 21 jela kwa jukumu lao la mapinduzi hayo yaliofeli,ikimuhukumu waziri wa ulinzi Cyrille Ndayirukiye na majenerali wengine watatu kifungo cha maisha ,wengine tisa kifungo cha miaka 30 pamoja na wanajeshi wanane waliopewa kifungo cha miaka 5.

Waendesha mashtaka wamesema katika taarifa kwamba hawakuridhika na hukumu hiyo na watu saba walioachiliwa na mahakama hiyo ni sharti washtakiwe upya kulingana na ripoti za AFP.