Muslim Brotherhood waponea kunyongwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mamia ya wafuasi wa Muslim Brotherhood wamesalia korokoroni

Mahakama ya rufaa nchini Misri imebatilisha hukumu ya kifo dhidi ya wanachama 140 wa vuguvugu la Muslim Brotherhood.

Wafuasi hao walihukumiwa kunyongwa kwa kukishambulia kituo cha polisi mjini Cairo mwaka 2013. Mahakama hiyo imetaka kesi dhidi ya watu hao kufunguliwa upya ambapo walipatiakana na hatia ya mauaji ya watu 13 wengi wao wakiwa ni maafisa wa polisi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Viongozi wakuu wa Muslim Brotherhood wamewekwa korokoroni

Shambulio hilo lilifanyika siku moja ambapo mamia ya watu waliuawa baada ya polisi kuvunja kambi za waandamanaji wa Muslim Brotherhood.

Walikua wakipinga mapinduzi ya kijeshi dhidi ya utawala wa Rais Mohammed Morsi aliyeonekana kuunga mkono sera za kiisilamu.