Makasha 18 ya sukari yakamatwa Mombasa

Image caption Mapipa ya Ethanol yakimwagwa baharini

Makasha 18 ya sukari yaliokamatwa katika bandari ya Mombasa yakielekea Uganda yamefunguliwa na sukari hiyo kumwagwa baharini.

Mamlaka ya ushuru nchini Kenya imesema kuwa bidhaa hiyo haikulipiwa na kwamba haikuwa bora kwa afya ya binaadamu.

Kulingana na na taarifa iliotiwa saini na kamishna wa mamlaka hiyo John Njiraini, Mamlaka hiyo pia imekamata makasha mengine 63 yaliojaa mapipa ya Ethanol.

Image caption Magunia ya sukari yakimwagwa baharini bandarini Mombasa

Njiraini amesema kuwa vita dhidi ya biashara haramu vitaimarishwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa wenye biashara hizo wanashtakiwa.

Mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi alishuhudia mapipa hayo ya Ethanol iliokuwa ikitoa harufu mbaya yakimwagwa baharini.

Wafanyikazi wanasema kuwa wana mpango wa kupunguza ukali wa mafuta hayo ya Ethanol kabla ya kuyamwaga baharini.

Image caption Mapipa ya Ethanol

Ethanol hutumiwa kutengeneza pombe.