Porsche:Hatutengezi magari yanayojiendesha

Haki miliki ya picha AFP
Image caption gari aina ya Porsche

Porsche haina mpango wa kutengeza magari yanayojiendesha bila dereva ,kinyume na kampuni nyengine za kutengeza magari ambazo ziko katika harakati ya kuanzisha magari hayo,kulingana na mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo.

Oliver Blume ameliambia gazeti la Ujerumani la Westfalen-Blatt kwamba watu walitaka kuendesha Porsche wenyewe binafsi.

Ameongezea kuwa kampuni hiyo haina mpango wa kushirikiana na kampuni yoyote ya kiteknolojia.

Wachanganuzi wa Boston Consulting Group wanatabiri kwamba kufikia mwaka 2025,asilimia 13 ya magari yatakuwa na vifaa huru.

Hatahivyo amesema kuwa kampuni ya Porsche ina mpango wa kuzindua gari la kielektroniki lenye kasi ya kilomita 50 ambalo litakuwa sokoni mwanzoni mwa mwaka 2018.

Porsche pia ina mpango wa kutumia yuro bilioni moja katika uzalishaji wa magari ili kujenga gari aiana ya Mission E ikiwa ndilo gari lake la kwanza la kielektroniki, hatua ambayo inalinganishwa na ile ya kampuni ya Volkswagen ya kuongeza magari yake ya kielektroniki wakati ambapo pia inakabiliwa na sakata ya magari yanayotoa moshi mwingi.