US: Wagombea sasa waelekea New Hampshire

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Uchaguzi wa mchujo jimboni New Hampshire

Wanachama wa Republican na Democrats nchini Marekani wanaopigania tiketi za vyama vyao tayari kwa uchaguzi wa urais nchini Marekani wameanza kuwasili katika jimbo la New Hampshire ambapo uchaguzi mwengine utafanyika.

Walioshinda katika kamati za wabunge za Iowa walikuwa Sineta Ted Cruz wa chama cha Republican na Hillary Clinton wa Democrats.

Bw.Cruz alishinda licha ya kuwa nyuma katika kura ya maoani huku Bi.Clinton akimshinda sineta Bernie Sanders kwa asilimia 0.2.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bernie Sanders akikosoana na Hillary Clinton katika mjadala jimboni New Hampshire 2005

Jimbo la New Hampshire linaonekana kuwa na changamoto tofauti kwa vyama hivyo.Jimbo hilo lenye watu wa msimamo wa kadri na wasio na wasiofuata dini huenda likawa changamoto kubwa kwa bwana Cruz wakati mchujo huo utakapofanyika mnamo tarehe 9 mwezi Februari.

Donald Trump,ambaye amekuwa kifua mbele kwa upande wa chama cha Republican anatarajiwa kufanya vyema zaidi ya Iowa ambayo mchujo wa kwanza ulifanyika.

Upande wa Democrats,Bw.Sanders anaonekana kuwa na fursa ya kuwa nyumbani dhidi ya Bi Clinton,akiwa sineta wa jimbo jirani la Vermont.

Hata kabla ya ushindi mdogo wa Bi.Clinton kutangazwa rasmi,Bw.Sanders alikuwa amepanda katika lori moja akisalimiana na mashabiki katika mji wa Bow jimbo la New Hampshire.

Haki miliki ya picha
Image caption Mchujo wa uchaguzi wa Urais

Akiuambia umati huo kwamba kampeni yake imeushangaza ulimwengu huko Iowa,ameahidi kwamba itaushangaza tena ulimwengu katika Jimbo la New Hampshire.

Katika jimbo hilo,Bi Clinton alitangaza ushindi akisema kuwa anaamini kwamba anaelekea kupata ushindi mwengine katika jimbo la New Hampshire baada ya kuibuka mshindi Iowa.

''Nimeshinda na kupoteza huko, na ni vizuri kushinda'',alisema akiangazia alipopoteza katika jimbo hilo mwaka 2008.