Zika:Dharura yatangazwa Florida Marekani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Virusi vya Zika vinakisiwa kusambaa kwa njia ya kujamiiana

Gavana wa jimbo la Florida, Rick Scott ametangaza hali ya dharura katika Kaunti nne kutokana na virusi vya Zika.

Kesi tisa za ugonjwa huo zimegunduliwa jimboni Florida.

Maafisa wa afya wanaamini kuwa maambukizi hayo yametokea baada ya watu kusafiri kwenye nchi zilizoathirika.

Virusi vya Zika vinavyosababisha dosari kwenye ubongo kwa watoto,vimekuwa hoja inayozungumzwa sana ulimwenguni.

Virusi hivi husambazwa na mbu, lakini wachunguzi wa maswala ya afya wanasema huenda virusi hivi vinasambazwa kwa njia ya kujamiiana.

Maafisa wa masuala ya afya nchini Marekani wamesema mtu mmoja jimboni Texas aliathirika na virusi vya Zika kwa njia ya kujamiiana, hlo ni tukio la kwanza la ugonjwa huo kutokea nchini Marekani.