Picha 10 za kusaidia kuelewa madhara ya kansa duniani

Tarehe 4 Februari ni Siku ya Saratani Duniani, siku inayotumiwa kuhamasisha watu zaidi kuhusu ugonjwa huu pamoja na kukabiliana na dhana potufu kuhusu ugonjwa huo ambao umeathiri watu wengi sana duniani.

Ni miongoni mwa magonjwa yanayoua watu wengi duniani, na mabilioni ya pesa yametumiwa kukabiliana nao.

Saratani si ugonjwa mmoja, ni magonjwa zaidi ya 200, kila ugonjwa ukiwa na dalili zake tofauti na njia za kuupia na pia kutibu.

Shirika la Afya Duniani linasema visa vya kansa vitaongezeka kwa 70% katika kipindi cha miaka 20 ijayo.

Hii ina maana gani? Hapa kuna michoro 10 ya kusaidia kuelewa kuenea kwa ugonjwa wa saratani duniani kwa sasa.

1.

2.

Aina za saratani zinazopatikana sana duniani hazijabadilika sana katika kipindi cha miaka 40 iliyopita, wataalamu wa kansa kutoka Cancer Research UK wanasema.

Aina nne za saratani zinazotatiza watu sana – saratani ya mapafu, matiti, matumbo na tezi dume, husababisha zaidi ya visa 4 katika 10 vya saratani kote duniani (42%) kote duniani, kwa mujibu wa mradi wa Globocan.

Mradi wa Globocan ni hazina data ya habari kuhusu saratani ambayo husimamiwa na Chama cha Kimataifa cha Sajili za Saratani.

Saratani ya mapafu ndiyo inayopatikana sana miongoni mwa wanaume, huku saratani ya matiti ikipatikana zaidi miongoni mwa wanawake.

3.

KUISHI NA SARATANI

169.3 Mamilioni ya miaka

ya maisha mema yanayopotea kutokana na kansa duniani kila mwaka

 • Watu milioni 32.6 wanaishi na saratani duniani (wale waliopatikana na saratani katika miaka mitano iliyopita waliokuwa hai kufikia mwisho wa 2012, takwimu za karibuni zaidi)

Getty

4.

Ripoti ya Saratani Duniani iliyotayarishwa na Shirika la Afya Duniani inaonyesha kwamba zaidi ya 60% ya visa vipya vya saratani duniani vinatokea Afrika, Asia na Amerika Kusini na Kati.

Maeneo hayo yanachangia vifo 70% vinavyotokana na kansa duniani.

Kuwepo kwa visa vya kansa hata hivyo hakuendani sambamba na vifo, hata hivyo. Baadhi ya maeneo yana rasilimali bora za kuhudumia wanaougua saratani na kuongeza uwezekano wao wa kuishi.

Kwa mfano, Ulaya na Amerika Kaskazini zinashuhudia kiwango cha chini cha vifo kutokana na saratani, huku Asia na Afrika zikiwa na kiwango cha juu cha vifo.

5.

6.

Tukiangalia idadi ya visa vya saratani katika taifa, kiwango cha juu zaidi cha visa vya saratani kwa wanaume na wanawake kipo Denmark, ambapo watu 338 katika kila watu 100,000 walipatikana na saratani mwaka 2012.

NCHI 5 ZINAZOONGOZA

KWA KUWA NA VISA VINGI VYA SARATANI

1. Denmark

Watu 338.1 katika kila watu 100,000

 • 2. Ufaransa 324.6

 • 3. Australia 323.0

 • 4. Ubelgiji 321.1

 • 5. Norway 318.3

Thinkstock

Denmark inafuatwa na Marekani, Ireland, Korea, Uholanzi na New Caledonia.

Eneo la Mashariki ya Kati, Israel ndilo taifa ambalo lina kiwango cha chini zaidi, aikiwa nambari 19 katika orodha ya mataifa 50 bora.

Barbados (27) na Uruguay (33) ndiyo mataifa yenye viwango vya kushtua zaidi barani Amerika nyuma ya Marekani na Canada. Cuba, Argentina na Puerto Rico pia zimo kwenye orodha ya nchi 50 zinazoongoza.

7.

SARATANI na MAENDELEO

57% ya visa vyote vya kansa

hutokea katika nchi ambazo hazijaendelea - licha ya kwamba saratani huchukuliwa sana kuwa tatizo la nchi zilizoendelea

 • 43% ya visa vyote duniani vinaripotiwa nchi zilizoendelea

Getty

8.

Hatari zinazodhaniwa kusababisha saratani kote duniani ni sawa, wataalamu wanasema.

HATARI ZINAZOHUSIANA NA SARATANI

Theluthi moja

ya vifo vinavyosababisha na kansa hutokana na mambo

4

ya mitindo na ulaji chakula

 • 1. Kutumia tumbaku

 • 2. Chakula na unene

 • 3. Pombe

 • 4. Kutofanya mazoezi

Uvutaji wa sigara na matumizi ya tumbaku unaongoza, ikichangia 20% ya vifo vinavyosababishwa na saratani duniani.

Unywaji pombe ndio unaoongoza kwa kusababisha vifuo Ulaya na Amerika, huku kutokula vyakula vifaavyo pamoja na unene vikianza kuchangia vifo zaidi katika nchi za mapato ya chini na wastani.

Pia, maambukizi yanasababisha 18% ya visa vya saratani, kiwango hiki kikiwa zaidi katika maeneo maskini.

9.

KUPATA DAWA ZA KUPUNGUZA MAUMIVU

kwa wanaougua kansa duniani

99%

ya vifo vyenye uchungu na bila kutibiwa hutokea nchi zinazoendelea

 • 90% ya dawa za kupunguza mauamivu duniani hutumiwa Australia, Canada, New Zealand, Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya

 • Chini ya 10% ya dawa hizo hutumiwa na 80% ya watu hao wengine duniani

Getty

10.

SARATANI SIKU ZIJAZO

Wataalamu wanabashiri nini

Ongezeko la 70%

la visa vipya vya saratani duniani katika miongo miwili ijayo

 • Milioni 21.4 Wagonjwa wapya kufikia 2032, ongezeko kutoka milioni 14.1 mwaka 2012

Thinkstock