Uhaba wa mikate wakumba Nigeria

Image caption Kuna utashi mkubwa sana wa waokaji mikati nchini Nigeria.

Kuna uhaba mkubwa sana wa waokaji mikate nchini Nigeria.

Hili limetokana na mgomo ulioitishwa na wawakilishi wa waokaji mikate katika maeneo mengi ya Nigeria.

Mkate ni haba katika miji wa kaskazini wa Nigeria haswa jimbo la Kano.

Kwa sasa wenyeji wanapiga foleni ndefu mno ili angalau wakapate mkate katika maduka machache yaliyowazi.

Image caption Mkate ni haba katika miji wa kaskazini wa Nigeria haswa jimbo la Kano.

Kano Bakers Association wanasema waokaji mikate wengi wamekuwa wakipata hasara kwa sababu ya kupanda kwa gharama, na nia yao kugoma angalau ni kuwasilisha ujumbe kwa viongozi kuwa haina faida tena na maisha ya watu wengi wanaotegemea biashara hiyo imo hatarini.

"Bei ya viungo vyote ikiwa ni pamoja na unga, sukari na imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 20% katika miezi mitatu iliyopita.

Hii wanasema imetokana na upungufu mkubwa wa fedha za kigeni inayoikumba Nigeria " alisema msemaji wake Kabiru Hasan.

Hapo nyuma ,Kwa dola zipatazo senti 50 kwa kawaida huwa unaeweza kupata kifungua kinywa chenye hadhi ya wastani yenye mkate na mayai katika maeneo mengi ya Kano kaskazini mwa Nigeria.

Image caption Bei ya viungo vyote ikiwa ni pamoja na unga, sukari na imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 20% katika miezi mitatu iliyopita.

Ni chakula kikuu kwa watu milioni tisa wanaoishi katika eneo hilo.

Bei za bidhaa kila siku zinaongezeka kwa sababu serikali imeweka vikwazo dhidi ya upatikanaji wa fedha za kigeni, hivyo imekuwa vigumu kuingiza bidhaa.

Maisha ya wauzaji chai na wateja wao yameathirika pakubwa na mgomo.

Wanasema hali ikiendelea hivi wengi watalazimika kwenda kazini bila ya kinywa kawaida.