Je mtu alitupwa ndege ikiwa angani Somalia ?

Image caption Je mtu alitupwa nje ndege ikiwa angani Somalia ?

Polisi nchini Somalia wanafanya uchunguzi kujua iwapo mwili uliopatikana karibu na uwanja wa ndege wa Mogadishu ulitupwa kutoka angani.

Polisi wanashuku ndege moja iliyotua katika uwanja huo Jumanne ikiwa na shimo .

Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la Daallo ililazimika kutua kwa dharura baada baada ya mlipuko ulioacha shimo ubavuni mwake.

Awali ilisemekana kuwa abiria wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo walipatikana lakini baada ya buda ikabainika kuwa huenda mtu mmoja alitupwa nje kutokana na tofauti ya hewa ndani na nje ya ndege hiyo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rubani wa ndege hiyo anasema huenda ilikuwa ni bomu.

Wenyeji wa kitongoji kimoja karibu na uwanja wa ndege wanasema walipata mwili wa mtu mmoja unaoshukiwa kuwa wa abiria huyo.

Polisi wanaosimamia shughuli za ndege wameanzisha uchunguzi wa kina wa mwili huo kubaini kilichosababisha kifo chake.

Vilevile kunahofu kubwa kuhusiana na kilichosababisha mlipuko huo mkubwa muda mchache tu baada ya ndege hiyo kupaa kutoka uwanja huo wa kimataifa wa Mogadishu.

Rubani wa ndege hiyo anasema huenda ilikuwa ni bomu.

Maafisa wanaosimamia maswala ya usafiri wa ndege hata hivyo wanapinga wakidai kuwa hawajapata ushahidi wa aina yeyote kuwa kulikuwa na bomu ndani ya

ndege hiyo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la Daallo ililazimika kutua kwa dharura baada baada ya mlipuko ulioacha shimo ubavuni mwake.

Abiria hao hata hivyo wanakila sababu ya kumshukuru mungu kwani ndege hiyo ilipata nafasi ya kutua kwa sababu haikuwa imepaa juu angani.

Kwa mujibu wa maafisa wanaosimamia safari za ndege, laiti ndege hiyo ingekuwa imepaa juu angani basi ingevunjika ikiwa juu na kusababisha hasara na maafa makubwa mno.

Wapiganaji wa Al-Shabab wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara wakilenga uwanja huo wa kimataifa wa Mogadishu.

Ni ndege chache tu ambazo bado zinaendesha shughuli zake kutoka uwanja huo wa ndege.