Upimaji wa ubikira wakosolewa Afrika Kusini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Upimaji wa Ubikira Afrika Kusini

Waziri mmoja wa Afrika Kusini ameshtumu kuwa kinyume cha sheria ufadhili wa elimu ya wasichana wanaopita kipimo cha ubikira.

Mwezi Uliopita,Manispaa ya uthukela katika jimbo la Kwazulu Natal nchini Afrika Kusini ilisema itawapa zawadi wanafunzi 16 wa kike kwa masharti kwamba wasalie mabikira.

''Mpango huo ulilenga kupunguza maambukizi ya virusi vya HIV na mimba za mapema miongoni mwa wasichana'',alisema Meya Dudu Mazibuko.

Katika taarifa ya gazeti la Daily Maverick,waziri wa maendeleo ya kijamii Bathabile Dlamini alielezea upimaji wa ubikira kama usiowezekana,mchafu na ukiukaji mkubwa na haki za kibiniaadamu.

''Kujamiana kwa mara ya kwanza hakutakikani,licha ya hilo kuna unyanyapaa miongoni mwa wasichana ambao hufeli kipimo hicho'',alisema,akiutaja mpango huo kama ''kosa la kingono''.

Bi. Dlamini ,ambaye ni kiongozi wa chama tawala cha ANC upande wa wanawake ndio kiongozi mwenye hadhi ya juu kupinga kipimo hicho.