Kisa cha maambukizi ya Zika charipotiwa Ulaya

Zika Haki miliki ya picha AP
Image caption Virusi vya Zika vinasababisha watoto kuzaliwa na vichwa vidogo

Kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya Zika kimethibitishwa barani Ulaya.

Mwanamke mmoja nchini Uhispania, ambaye alirejea nchini humo majuzi kutoka nchini Colombia amepatikana na virusi hivyo.

Wizara ya afya inasema inaaminika kwamba aliambukizwa virusi hivyo akiwa nchini Colombia.

Virusi vya Zika vinaaminika kusababisha watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo na ubongo uliodumaa.

Virusi hivyo vinaenea kwa kasi mataifa ya Amerika na Shirikisho la Afya Duniani (WHO) limetangaza dharura ya kimataifa duniani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Virusi vya Zika vinaenezwa sana na mbu

Virusi hivyo vinaenezwa sana na mbu ingawa kisa cha maambukizi kutokana na kushiriki mapenzi kimethibitishwa katika jimbo la Texas, Marekani.