Sanders na Hillary Clinton wachuana

Haki miliki ya picha
Image caption Hillary Clinton na Bernie Sanders kuchuana kwenye mjadala

Waliosalia katika kinyang'anyiro cha kutaka kuwania kupeperusha bendera ya urais kupitia chama cha Democratic nchini Marekani, Hillary Clinton na Bernie Sanders wanafanya mdahalo wao wa kwanza wa ana kwa ana kuelekea katika kura ya maoni itakayofanyika katika Jimbo la New Hampshire.

Sanders amemlaumu mpinzani wake kwa kuwa kupata mteremko, tuhuma ambazo Bi Clinton mwenyewe amezibeza na kusema kuwa anajaribu kupata uteuzi wa kuwa mgombea wa kwanza wa kike.

Wanasiasa hao pia wamekwaruzana kuhusu fedha za kampeni na fedha za huduma ya afya na elimu.

Mchuano huo wa Democrat ulipamba moto baada ya Sanders kuunyemelea kwa karibu mno ushindi wa aliyekuwa waziri wa mambo ya nje katika mchuano uliofanyika huko jimboni IOWA.