Man City yachapwa 3-1 na Leicester City

Image caption Kocha Claudio Ranieri wa Leicester akionyesha kidole cha ushindi kwa timu yake.

Viongozi wa ligi ya Uingereza Leicester wamewashangaza wapinzani wao wa karibu katika ligi hiyo Manchester City baada ya kuwacharaza 3-1 katika uwanja wa Etihad na hivyobasi kupanda juu wakiwacha pengo la pointi sita.

Robert Huth alifunga kona iliopigwa na nyota wa timu hiyo Mahrez ,likiwa ni bao lililoiweka kuiweka kifua mbele timu yake.

City ilitishia kusawazisha bao kwa kuvunja safu ya ulinzi ya Leicester huku mabeki wao wakionekana kutatizwa na washambuliaji wa Leicester.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Raheem Sterling

Mahrez alifunga bao la pili huku Huth akifunga bao la tatu na kufanya mambo kuwa 3-0 kabla ya Sergio Aguero kuipatia City bao la kufutia machozi kunako dakika za mwisho.

Leicester ilikuwa imeishinda Tottenham iliopo katika nafasi ya tatu lakini ni ushindi huu dhidi ya Manchester City ambao umekuwa muhimu sana kwao.

Mbweha hao sasa wamechukua pointi 28,licha ya kupokonywa ushindi wa sita katika mechi zao saba.