US:Picha 198 za wafungwa walionyanyaswa

Image caption Pentagon

Takriban picha 200 zinazohusishwa na madai ya unyanyasaji uliotokelezwa na wanajeshi wa Marekani nchini Iraq na Afghanistan muongo mmoja uliopita zimetolewa na Pentagon.

Picha hizo zilitolewa kufuatia ombi la uhuru wa habari lilitolewa na Muungano wa wanaharakati nchini Marekani ACLA.

Picha hizo zinaonyesha michubuko na alama za kukatwa katika mikono ya wafungwa na miguu.

Kashfa hiyo ya unyanyasaji ilizuka mwaka 2004 wakati picha za kushangaza za wanajeshi wa Marekani wakiwanyanyasa kingono wafungwa wa Abu Ghraib nchini nchini Iraq.

Hakuna hata picha moja iliotolewa siku ya Ijumaa iliwahusisha wafungwa hao wa Abu Ghraib ama hata katika kituo cha kuwazuiia wafungwa cha Guantanamo Bay nchini Cuba,Pentagon imesema.

Msemaji amesema kuwa picha hizo zilitoka kwa wachunguzi huru wa uhalifu kuhusu madai ya utovu wa nidhamu wa maafisa wa wanajeshi wa Marekani.

Takriban madai 14 yalithibitishwa na kusababisha maafisa 65 kuadhibiwa.