Wanajeshi wa serikali wakomboa Merka, Somalia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi wa Umoja wa Afrika

Ripoti zinasema kuna mapigano nje ya Bandari ya Somalia, ambayo hapo jana ilitekwa na wapiganaji Waislamu wa al-Shabab.

Msemaji wa jeshi la Somalia, (Abdirisak Mohamed) alieleza kuwa wanajeshi wa serikali, wakisaidiwa na askari wa kuweka amani wa Umoja wa Afrika, wameikomboa bandari ya Marka, kilomita mia moja kusini magharibi mwa mji mkuu, lakini habari hizo haziku thibitishwa na wengine.

Kikosi cha AU, ambacho kimedhibiti bandari hiyo kwa miaka mitatu sasa kiliondoka jana pamoja na wanajeshi wa Somalia na hivyo, kuwezesha al-Shabab kuingia mji huo wa Marka.

Haki miliki ya picha d
Image caption Alshabab

Picha zimeonekana katika mitandao ya al-Shabaab, zikionyesha wapiganaji hao wakipandisha bendera yao katika mji huo, na kuhutubia watu.