Afrika ya Kati yahitaji amani zaidi

Shirika la kimataifa la Amnesty limeitaka umoja wa kimataifa kuongeza nguvu kwa wanajeshi wake wa kulinda amani katika Jamuhuri ya Afrika ya kati.

Vikundi vya kutetea haki za binadamu vinasema kuna upungufu kwenye nguvu kazi na vitendea kazi ambavyo vinapelekea raia kuwa katika hali ya hatari zaidi katika mgogoro huo wa kivita.

Shirika hilo linasema,jeshi la umoja wa mataifa limeshindwa kuzuia milipuko iliyotokea katika mji mkuu wa Bangui mwezi septemba ambapo ulisababisha watu zaidi ya ishirini na tano kuuwawa.

Afrika ya kati ambayo imekuwa katika mgogoro tangu pale ambapo kikundi cha waasi wa kiislamu wa Seleka kutoka madarakani mwaka 2013 ,na kuchochea ghasia ya kulipiza kisasi kwa kikundi cha wapiganaji cha kikrosto.

Nchi hiyo itarudia kufanya uchaguzi kwa kupiga kura ya kumchagua rais mpya ndani ya wiki moja , na kampeni zinazotarajiwa kuanza siku ya Jumatatu.