Haiti kuunda serikali ya mpito

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Haiti kuunda serikali ya mpito

Wanasiasa nchini Haiti wametia sahihi makubaliano ya dakika za mwishi ya kubuni serikali ya mpito siku moja kabla ya rais Michel Martelly kuondoka madarakani bila ya kuwepo mrithi aliyechaguliwa.

Makubaliano hayo yaliyotiwa sahihi na marais wa bunge zote mbili yanaizuia nchi kutokana na kutumbukia katika hali ya kutokuwa na kiongozi.

Shughuli ya kumchagua mrithi wa bwana Martelly ilihairishwa mwezi uliopita kutokana na hofu ya kutokea ghasia na kuwepo kwa udanganyifu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shughuli ya kumchagua mrithi wa bwana Martelly ilihairishwa mwezi uliopita kutokana na hofu ya kutokea ghasia na kuwepo kwa udanganyifu.

Chini ya makubaliano hayo bunge litamchagua rais wa kipindi cha mpwito ambaye atahudumu mwa muda wa miezi minne.

Uchaguzi wa nchi hiyo sasa umepangiwa kufanyika tarehe 24 mwezi Aprili.