Kasisi anayepinga dhulma akaidi amri ya Vatican

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kasisi Peter Sanders amekosoa taarifa kutoka Vatican ambayo inasema kwa alikuwa akienda likizoni.

Mwanachama mashuhuri wa tume inayoshughulikia masuala ya unyanyasaji wa kimapenzi unaofanywa na makasisi amepinga vikali jinsi anavyotendewa na makao makuu ya kanisa Katoliki huko Vatican.

Peter Sanders amekosoa taarifa kutoka Vatican ambayo inasema kwa alikuwa akienda likizoni.

Anasema kuwa hawezi kamwe kuondoka katika tume hiyo na kuongeza kuwa atazungumzia hatma yake na yule aliyemteua ambaye ni kiongozi wa kanisa katoliki papa Francis.

Bwana Sanders binafsi alinyanyaswa kimapenzi akiwa mtoto na amelikosoa kanisa katoliki kwa kufunika visa ya unyanyasaji na kushindwa kuwaadhibu makasisi husika.