Beyonce alivyoteka jukwaa Super Bowl

Beyonce Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wengi walibaki wakizungumza kuhusu utumbuizaji wa Beyonce

Kipindi cha utumbuizaji wakati wa mapumziko Super Bowl kilifaa kuwa wakati wa Coldplay kung’aa, lakini Beyonce ndiye aliyewika.

Bendi hiyo ya Uingereza ilianzisha kipindi hicho cha burudani cha dakika 13 kwa nyimbo zao maarufu kabla ya Bruno Mars na Queen B kujiunga nao jukwaani.

Haki miliki ya picha Getty

Beyonce alipanda jukwanii kutumbuizwa kwa wimbo wake mpya Formation, Bruno Mars na Mark Ronson wakitumbuiza kwa Uptown Funk.

Wengi mara moja walianza kujadili jinsi Beyonce alivyotumia utumbuizaji wake kutoa ujumbe kuhusu haki za watu weusi.

Haki miliki ya picha Getty

Wanenguaji viuno wake walikuwa wamevalia mavazi yaliyofanana nay a kundi la kisiasa la Black Panthers, na walijipanga kwa umbo la X, jambo ambalo linaonekana kumrejelea mwanaharakati mtetezi wa haki za watu weusi Malcolm X.

Mamake Beyonce pia alipakia mtandaoni picha ya bintiye na wanenguaji wake, wote wakiwa wamepiga saluti ya kuashiria nguvu za watu weusi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kunao hata hivyo ambao hawajafurahishwa na video yake ya Formation

Kunao baadhi, hata hivyo, ambao hawakufurahishwa na mwanamuziki huyo na walikuwa wamewataka watu kususia utumbuizaji wake katika Super Bowl.

Kundi hilo lilianza kampeni hiyo punde baada ya kutolewa kwa video ya Formation.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Beyonce akiwa na Chris Martin na Bruno Mars

Mwanamke mmoja aliandika kwenye Facebook yake: “Kama mke wa afisa wa polisi, video yote inaniudhi.

Beyonce alitumia hafla hiyo kutangaza kuwa karibuni ataanza ziara yake ya kutumbuiza mashabiki miji mbalimbali duniani.

Haki miliki ya picha Getty