Hong Kong vurugu zatawala

Haki miliki ya picha BBC Chinese

Vurugu zimetokea katika mji wa Hong kong,kitongoji cha Mong kok wakati polisi wakifanya operesheni katika maduka yanayouza vyakula haramu.

Fujo hizo zilianza wakati wataalamu wa usafi na chakula walipojaribu kuondoa vibanda ambavyo vilikuwa barabarani, wafanyabiashara wenye hasira kali walianza kurushia mawe polisi na kuwasha moto barabarani ili kupinga kitendo hicho.

Hong kong ambayo bado inasheherekea sherehe za mwaka mpya zilizoanza jana na kuchukua siku tatu za mapumziko. Maduka ya mitaani yanayouza vyakula na vinyaji ni kawaida kwa wao kuuza bidhaa bila kuwa na vibali halali.