Dalili za uhai katika mgodi ulioporomoka A.Kusini

Image caption Jamaa za wachimbaji mgodi wa Lily Mine Afrika Kusini

Kuna dalili ya uhai kutoka katika mgodi wa dhahabu kufuatia ajali wiki iliyopita, ambapo watu watatu walifunikwa waokoaji anasema.

Wachimbaji mgodi watatu wamekwama katika chumba cha taa,baada ya mgodi huo kuporomoka kufuatia kisa ambapo jumba moja lililoko karibu na mgodi huo lilipoporomokea mgodi huo siku ya ijumaa.

Kundi la waokoaji linasema kuwa walisikia mlio wa ukuta ambayo huwa ni ishara ya mawasiliano kati ya wachimba mgodi wakiwa hatarini.

Ishara hiyo ya mawasiliano imeinua matumaini ya wenye mgodi huo kuwa wachimbaji mgodi walioko ardhini wangali hai.

Wafanyakazi zaidi ya 70 wa mgodi huo walifaulu kutoroka kutoka chini ya ardhi kwa kutumia njia maalum ya dharura baada ya ajali hiyo kutokea Ijumaa katika Lily Mine karibu na mji wa kaskazini mashariki wa Barberton .

Ajali hiyo ilisababishwa na jumba lililoporomokea mgodi huo na kusababisha tani kadhaa za kifusi kuharibu mgodi huo na kufunikia wafanyikazi ardhini.