Wahamiaji zaidi wafa maji wakienda Ulaya

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wahamiaji wanaendelea kufa maji wakijaribu kuingia Ulaya

Mashua mbili zilizokua zikielekea Ugiriki zimezama karibu na Uturuki na kuwaua wahamiaji 33. Hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uturuki.

Taarifa zinasema wahamiaji 22 walizama karibu na kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos. Wengine 11 walizama kusini kwa Uturuki katika mkoa wa Izmir.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Wengi wa wahamiaji wanaozama ni raia wa Syria wanaokimbia vita

Wahamiaji 374 wamekufa maji mwaka huu wakati wakijaribu kuingia Ulaya.Shirika la wahamiaji duniani IOM linasema wengi wamekufa wakielekea Ugiriki, njia inayotumiwa na wahamiaji wengi kuingia Ulaya.

Taarifa hizi zinajiri wakati Chancela wa Ujerumani Angela Merkel amewasili Uturuki kujadili jinsi ya kuthibiti idadi ya wahamiaji wanaojaribu kuingia Ulaya.Uturuki imewazuia maelfu ya raia wa Syria wanaokimbia mashambulizi ya jeshi la serikali katika mji wa Aleppo.