Wanafunzi 43 Mexico bado ni utata

Haki miliki ya picha AFP

Ripoti mpya inayohusu kupotea kwa wanafunzi wapatao arobaini na watatu katika jimbo la Guerrero , nchini Mexico umebainisha kwamba hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa kuunga mkono upande wa serikali juu ya nini kilichowapata wanafunzi hao.

Utafiti huo ulioendeshwa kwa muda wa mwaka mmoja na watafiti wenye asili ya Argentina wakiwemo wanasayansi wanaoaminika nchini humo, wamegundua kwamba hakuna ushahidi wa vifaa vya kimaumbile vya kunasibisha na wanafunzi hao kwenye jaa la taka lililoko kwenye mji wa Cocula.

Serikali ya nchi hiyo imesema kwamba wanafunzi hao waliuawa na miili yao kuchomwa moto baada ya polisi kula rushwa na kuwakabidhi wanafunzi hao kwa genge la wahuni ambao walitekeleza mauaji hayo, ingawa kwa upande mwingine kuna taarifa kwamba timu ya watafiti hao wanadai kwamba huendi miili hiyo ikawa ya watu wengine.

Wazazi wa wanafunzi hao waliopotea wanaendesha kampeni ya kutaka kuruhusiwa kuingia katika kambi za kijeshi zilizo karibu na eneo hilo, ambao wanadai kwamba, huenda likawa na viashiria vya moja kwa moja mahali walipo watoto wao.